Login With OTAPP

Sign in with OTAPP

Sign Up With OTAPP

Create An Account
Tunapenda teknolojia yenye umuhimu kwa maisha ya kisasa kwa moyo wote

Otapp ni kampuni ya kiteknolojia yenye kutaka kufanya mambo makubwa, inayotengeneza mifumo ya kikompyuta, ni mwanzilishi wa mifumo ya tiketi za kimtandao katika Afrika yenye makao makuu nchini Tanzania.... Tokea kuanza kwetu kama moja ya kampuni inayotoa mfumo bora wa tiketi za mabasi mwaka 2014, tumekua kama mfumo utoao tiketi kimtandao lakini pia pasipokuwa na mtandao pia ambapo mtandao ukirudi au ukiwepo, taarifa hutumwa kwenye mfumo. Tunatoa huduma ya tiketi kwa ajili ya matukio, nyumba za filamu/sinema, mabasi, usafiri wa baharini, usafiri wa anga, usafiri wa treni, starehe n.k. Na malipo kwa tiketi zitokazo kwenye mfumo wetu hufanywa kwa kimtandao, kama inavyokubalika na kupendwa katika soko la sasa.

Read more

Kujisikia Vizuri… Uzoefu Mzuri… Utoshelevu Mkubwa Kabisa

Utoshelevu mkubwa kabisa: Kama mtoa tiketi za kimtandao mbunifu Tanzania, watumiaji wetu wanaweza kufurahia kupata huduma mbalimbali za tiketi zisizo na mipaka wakati huo huo wakinunua na kulipia kwa kupitia mfumo wetu. Wakati wanaotembelea tovuti yetu wanaokoa fedha na muda kwa kununua tiketi zao mtandaoni, tunawapa wamiliki wa biashara faida ya kulifikia soko pasipo kikomo na hivyo kuongeza mauzo.

Dhima Yetu


Dhima Yetu ni kuwa waumbaji wabunifu wa mifumo ya kiteknolojia ya kimtandao inayoongeza thamani.

Maono Yetu


Maono Yetu ni kutengeneza mifumo ya kibunifu ya teknolojia ya kimtandao kwa ajili ya kuwezesha shughuli za kibiashara kufanyika kiteknolojia na kuitumia nguvu ya teknolojia kuwezesha kuokoa muda na rasilimali.

Mwelekeo Wetu


Mwelekeo Wetu ni kuongoza katika kutengeneza na kutoa mifumo ya kiteknolojia ya kimtandao kwa ajili ya biashara na watu katika Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika.

Tunavyovithamini


Viwango Vya Kidunia

Kinachofanya mfumo wetu uwe kama ulivyo, pamoja na yote unayoweza kufanya ni kutengenezwa kwa kuunganishwa kwa lugha mbalimbali za kutengeneza mifumo ya kikompyuta kwa pamoja na hivyo unaweza kuunganishwa na mfumo wowote duniani.

Ubunifu na Teknolojia

Kila wakati tunataka kuboresha huduma zetu tunazotoa kulingana na mabadiliko ya teknolojia.

Uthabiti Wetu

Tuko thabiti kuhakikisha tunafikia matakwa na matarajio ya wateja wetu na kuona wameridhika.

Ubora

Tunatoa mfumo wa kuweka nafasi na kukata tiketi kimtandao ulio wa gharama nafuu na rahisi kuutumia.

Usiri

Biashara yetu inathamini usiri na kutotoa taarifa za siri za kibiashara za wateja wetu.

TIMU YA OTAPP


CEO
Rogers Mahanyu
COO
Joachim Ferdinand
Accountant
Janeth Christian
CTO

Otapp ni kampuni ya kiteknolojia yenye kutaka kufanya mambo makubwa, inayotengeneza mifumo ya kikompyuta, mwanzilishi wa mifumo ya tiketi za kimtandao katika Afrika. Jionee tulivyorahisisha kununua tiketi kimtandao.

Anuani

Regent business park,

Chini, Mikocheni,

Mtaa: Repoa. S.L.P. 12195,

Dar-Es-Salaam,Tanzania.

Blogu
@Blogu Angalia eneo hili kwa taarifa zaidi za matukio
5 minutes ago
Hakimiliki © Haki zote zimehifadhiwa | Sera ya usiri | Kuhusu | Vigezo na Masharti | Kutegemeza Mfumo & Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara na Majibu Yake